Kuhusu Uk Swahili Channel

Tunaamini kuwa watu wote hustawi kwa kuweza kutoa maoni na mawazo yao na kupata fursa ya ushirikiano na wengine wa karibu. Jamii hustawi kwa kufahamishwa ili waweze kushirikiana katika kutatua na kushughulikia maswala wanayopitia au kusherehekea mafanikio yao kwa pamoja.


Hivi sasa kuna idadi kubwa ya vituo vya Kiswahili ambavyo vinatangaza kutokea Tanzania na Kenya. Ingawa Idhaa hizi hutoa  taarifa na habari kwa wale walio kwenye diaspora, kuna upungufu wa habari ambazo zinatoka kwenye diaspora. Kusudio la Idhaa hii ya youtube ni kutoa habari, mahojiano, Makala na hati ambazo ni muhimu kwa jamii ya Kiswahili katika sehemu zote za ulimwengu. Kwa wale ambao hawapati utandawazi wa maswala ya nje ya nchi zilizopo Afrika Mashariki, watapata fursa ya kuelewa mafanikio na changamoto zinazowakuta waswahili waliyopo kwenye diaspora.  Pamoja na lengo hili idhaa hii itawaletea Makala maalum ambazo zitaweelimisha watazamaji kuhusu nchi zetu za Kiswahili, uzuri wake Pamoja na hali ya kimaisha inaowakabili wakazi wake.

Dhamira ni kutoa njia ambayo inasomesha, inasisitiza, inaleta furaha, kuchochea mawazo na kutoa mwongozo kupitia  vipindi vyake ambavyo ni kwa ajili ya watazamaji wa kila kizazi na umri.


Tuko tayari kupokea video kutoka kwa Mashabiki na watazamaji wetu kokote mliyopo duniani.


Tukuwe pamoja.

Waanzilishi

IMG-20200603-WA0006.jpg

Omar Hussein [Roy Snr]

Mwanzilishi & Mtangazaji

Omar Hussein ni mmoja wa waanzilishi wa UK Swahili Channel. Omar alipata shahada ya MEDIA katika chuo cha Ice Media kilichopo katika jiji la Leicester nchini Uingereza.

 

Pia amepata diploma katika masomo ya utangazaji wa radio na aliwahi kufanya kazi katika kituo cha Radio cha EAVA fm kilichopo jijini Leicester. Omar ni mtayarishaji na muongozaji wa baadhi ya vipindi vya UK Swahili Channel. 

Mbali na media Omar ni mmoja kati ya viongozi wa jumuiya ya An Noor hapa Leicester. Ni mpenda soka, masumbwi, UFC pamoja na riadha. Ni mpenzi kindakindaki wa timu ya Liverpool fc na pia ni mpenzi wa Dar Young Africans ya Tanzania.

Ali Abdallah [Tino]

Mwanzilishi & Mtangazaji

Ali Abdallah ni mmoja kati ya waanzilishi wa UK Swahili Channel. Amepata shahada ya diploma katika fani ya media huko South Leicestershire college, na pia ana cheti cha social care alichokipata Leicester college.

Ali ni mmoja kati ya wajumbe wa An Noor community akiwa kama care taker.

Vile vile ni mmoja kati ya wakongwe wanaounganisha vijana wa community katika kufanya mazoezi ya mpira wa miguu. Mbali ya soka Ali ni mpenzi wa masumbwi na michezo ya riadha.

Ali pia anapendelea kusafiri na kujuwa miji na tamaduni za mataifa memgine.

IMG-20200530-WA0001_edited.png
20200602_225314_edited_edited.png

Feisal Abasi [Fey]

Mwanzilishi & Mtangazaji

Feisal ni mmoja wa washiriki waanzilishi wa idhaa ya Kiswahili ya Uingereza. Amepata elimu yake ya sekondari jijini Leicester, ni miongoni mwa wale ambao hupunguza pengo kati ya vijana na wazee wa jamii ya Kiswahili. Amesomea mambo ya media na pia ana shahada katika Biashara na Usimamizi. Na ana ujuzi maalum katika marketing na branding kupitia kazi yake anayofanya na kampuni ya Light.Func. Yeye yuko mstari wa mbele katika ukuaji na maendeleo ya idhaa.


Ana masilahi mengi kama vile kuwa shabiki wa Arsenal mwenye uvumilivu, Mshabiki wa michezo ya aina mbali mbali, kusafiri na kukutana na watu wapya. Mbali na ucheshi wake wa kupenda kufurahisha yeye nii mwangalifu na anahisi kwamba ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja kama jamii kuhamasisha vizazi vijavyo na pia kutatua matatizo yanayotukabili hivi sasa katika jamii.

Timu Yetu

IMG-20200603-WA0002_edited.jpg

Mwatima Abdulla Haji

Matangazaji - Habari & Makala

Mwatima Abdulla Haji. Amepata elimu yake ya msingi na sekondari Jijini Zanzibar. Ni Muandishi wa Habari na mtangazaji wa UK Swahili Channel.
Amepata taaluma ya uandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa Habari na mawasiliano ya umma Zanzibar.
Ngazi ya Stashada. Mwatima anaipenda kazi yake yautangazaji, hata hivyo yeye ni mjasiriamali na mfanya biashara wa bidhaa katika sekta ya afya na urembo.
Vile vile ni mhamasishaji katka miradi tofauti inayozungumzia maendeleo kwa vijana
Ni mpenzi wa michezo, hupenda kuripoti habari za michezo nchini Zanzibar. Anaushabiki mkubwa wa timu ya  Zanzibar Heroes.
Mwatima yupo kwa ajili ya kuhakikisha watu wanapata kuelimika na kujua mengi kupitia UK Swahili Channel.

IMG-20200509-WA0002.jpg

Abdulrazaki Issa

Matangazi - Meza ya Hadithi

Abdulrazak Issa ni muandaaji wa kipindi cha Meza ya Hadith katika idhaa ya UK Swahili Channel. Kipindi ambacho kitakuwa kinachambua hadith sahihi za Rasulullah (SAW).
Abdulrazaki amepata elimu ya msingi na sekondari katika jiji la Dar es salaam. Pia amepata elimu na mafunzo ya dini ya kiislamu hapo  Dar es salaam.
Kwa sasa ni mwalimu wa madrasa na pia huwa anasomesha watu kwa kutumia njia ya mtandao
(online studies)
Mbali ya hayo pia huwa anapendelea kufanya vipindi vya sauti na video kwa kuelimisha jamii kwa kutumia mitandao. ya kijamii (Facebook na WhatsApp).
Hutumia muda wake wa mapumziko kucheza na kuangalia mchezo wa masumbwi. Na hutumia muda wa ziada katika kusoma vitabu.

WhatsApp%20Image%202020-06-03%20at%2018.

Abdelhameed Mjawiri Mjengo

Mhariri wa Video - Habari & Makala

Abdelhameed mjawiri mjengo ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na amepata elimu yake ya uandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa habari zanzibar ZJMMC.
Katika ngazi ya diploma na ni mtangazani anaejivunia na kuipenda kazi yake.
Madhumuni yake kuitangaza nchi yake kujulikana zaidi kimataifa, kupitia sanaa na utalii. 
Hutumia mda wake wa mapumziko kuangalia filamu na kutengeza filamu fupi.
Kuna mengi atakayowaleteeni kutoka UK Swahili Channel.

20200609_000008.jpg

Wadh-hat Abasi

Mtangazaji - kids Corner

Wadh-hat ana umri wa miaka 9 na mtangazaji wa Kids Corner. Alizaliwa jijini Leicester na wazazi wawili wa Kiswahili
na anafurahia safari za kwenda nchini
Tanzania kila mwaka ambapo yeye hutembelea babu na bibi zake.
Anaenda shule inayoitwa
Land of Learning. Wadh-hat ana mapenzi ya michezo ya kubahatisha, uchunguzi, masomo ya Kiisilamu na theolojia pia na maumbile, sayansi na hesabu. Yeye ni msemaji anayetarajiwa na amechaguliwa kuwasilisha mahojiano ya Kids Corner.
Tafadhalini jiungeni nae kuwasilisha sehemu tofauti za maisha yake,
pamoja na mafundisho ya Kiisilamu na mahojiano ya watoto wengine ndani ya jamii ya Kiswahili ya Uingereza.